Header Include

سواحلي ژباړه - علی محسن البرواني

سواحلې ژبې ته د قرآن کریم د معناګانو ژباړه، علی محسن البرواني ژباړلې ده

QR Code https://quran.islamcontent.com/ps/swahili_barawani

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ

Hatukukunjulia kifua chako?

Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani.
Hatukukunjulia kifua chako?

وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ

Na tukakuondolea mzigo wako!

Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,
Na tukakuondolea mzigo wako!

ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ

Ulio vunja mgongo wako?

Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.
Ulio vunja mgongo wako?

وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ

Na tukakunyanyulia utajo wako?

Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu.
Na tukakunyanyulia utajo wako?

فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi!

Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao.
Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi!

إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرٗا

Hakika pamoja na uzito upo wepesi.

Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe hujui), upo wepesi mwingi vile vile.
Hakika pamoja na uzito upo wepesi.

فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ

Na ukipata faragha, fanya juhudi.

Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe nafsi yako katika hayo.
Na ukipata faragha, fanya juhudi.

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب

Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.

Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.
Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.
Footer Include