Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Translated by Ali Muhsen Al-Berwani
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. [1]
[1] Ewe Muhammad! Hao wanao sema kwa kejeli, "Tusifie Mola wako Mlezi.": waambie: Yeye ni Mwenyezi Mungu wa pekee hapana mwenginewe, wala hana mshirika.
Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. [1]
ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. [2]
[2] Mwenyezi Mungu Mwenye kukusudiwa peke yake katika haja zote, na yote yanayo takikana.
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. [2]
لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ
Hakuzaa wala hakuzaliwa. [3]
[3] Hana mtoto wala hakuzaliwa na baba wala mama,
Hakuzaa wala hakuzaliwa. [3]
وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ كُفُوًا أَحَدُۢ
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. [4]
[4] Wala hana yeyote aliye mshabihi, au mfano wake.
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. [4]
مشاركة عبر