Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani
Translated by Ali Muhsen Al-Berwani
تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. [1]
[1] Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. [1]
مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. [2]
[2] Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. [2]
سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ
Atauingia Moto wenye mwako. [3]
[3] Ataingia katika Moto unao waka, aungue.
Atauingia Moto wenye mwako. [3]
وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ
Na mkewe, mchukuzi wa kuni, [4]
[4] Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).
Na mkewe, mchukuzi wa kuni, [4]
فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. [5]
[5] Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. [5]
مشاركة عبر