Савоҳилийча таржима - Али Муҳсин ал-Бервааний
Али Муҳсин ал-Бервааний таржимаси.
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo? [1]
[1] Unamjua anaye kanusha malipo na hisabu ya Akhera?
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo? [1]
فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ
Huyo ndiye anaye msukuma yatima, [2]
[2] Ukitaka kumjua basi ni huyo ambaye anaye msukuma yatima kwa nguvu, na anamtumilia mabavu, na anamdhulumu,
Huyo ndiye anaye msukuma yatima, [2]
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala hahimizi kumlisha masikini. [3]
[3] Na wala hahimizi kulishwa masikini.
Wala hahimizi kumlisha masikini. [3]
فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ
Basi, ole wao wanao swali, [4]
[4] Maangamio yatawashukia wanao sali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.
Basi, ole wao wanao swali, [4]
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ
Ambao wanapuuza Sala zao; [5]
[5] Maangamio yatawashukia wanao swali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.
Ambao wanapuuza Sala zao; [5]
ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ
Ambao wanajionyesha, [6]
[6] Ambao huonyesha kwa watu vitendo vyao, ili wapate cheo katika nyoyo za hao watu, na wasifiwe.
Ambao wanajionyesha, [6]
وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ
Nao huku wanazuia msaada. [7]
[7] Na huku wanazuia hisani zao na msaada wao kwa watu
Nao huku wanazuia msaada. [7]
مشاركة عبر