الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني
ترجمها علي محسن البرواني.
ٱلۡقَارِعَةُ
Inayo gonga! [1]
[1] AL-QAARIA'H, Inayo gonga, ni Kiyama, ambacho kinaanza kwa mpulizo wa mwanzo wa barugumu, na kinaishia itapo katwa hukumu baina ya watu.
Inayo gonga! [1]
مَا ٱلۡقَارِعَةُ
Nini Inayo gonga? [2]
[2] Kitu gani kilicho cha ajabu zaidi katika ukuu wake, na khatari zake na kitisho chake!
Nini Inayo gonga? [2]
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ
Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? [3]
[3] Na kitu gani kitacho kujuulisha hali ya AL-QAARIA'H katika kitisho chake juu ya nafsi za watu?
Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? [3]
يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; [4]
[4] Siku hiyo watu watakuwa kama vipepeo kwa wingi na kuhangaika kulia na kushoto, madhaifu na wanyonge!
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; [4]
وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! [5]
[5] Na milima itakuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na kuchambuliwa kwa kutapanyika vipande mbali mbali na kupeperuka katika anga huku na huku.
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! [5]
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, [6]
[6] Ama yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, mema yake yakapindukia kuliko maovu yake,
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, [6]
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. [7]
[7] Basi huyo atakuwa na maisha yatayo mridhisha mwenyewe, na nafsi yake itue.
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. [7]
وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, [8]
[8] Na ama ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, na maovu yake yakazidi kuliko mema yake,
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, [8]
فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٞ
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! [9]
[9] Basi makaazi yake yatakuwa Jahannamu.
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! [9]
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? [10]
[10] Na nini cha kukujuulisha ni nini Hawiya?
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? [10]
نَارٌ حَامِيَةُۢ
Ni Moto mkali! [11]
[11] Moto ulio mkali, hapana moto unao fikilia ukali wake, hata ukichochewa vipi na kutiwa kuni gani!
Ni Moto mkali! [11]
مشاركة عبر