Header Include

الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

ترجمها علي محسن البرواني.

QR Code https://quran.islamcontent.com/44/swahili_barawani

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ

Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, [1]

[1] Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha mambo yao.
Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu, [1]

مَلِكِ ٱلنَّاسِ

Mfalme wa wanaadamu, [2]

[2] Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote wafalme wao na maraia.
Mfalme wa wanaadamu, [2]

إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ

Mungu wa wanaadamu, [3]

[3] Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa ukamilifu atakavyo.
Mungu wa wanaadamu, [3]

مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ

Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, [4]

[4] Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.
Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas, [4]

ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ

Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, [5]

[5] Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.
Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu, [5]

مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ

Kutokana na majini na wanaadamu. [6]

[6] Kutokana na majini na wanaadamu.
Kutokana na majini na wanaadamu. [6]
Footer Include