Header Include

الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

ترجمها علي محسن البرواني.

QR Code https://quran.islamcontent.com/68/swahili_barawani

وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا

Naapa kwa jua na mwangaza wake! [1]

[1] Naapa kwa jua na mwangaza wake na kuchomoza kwake na kwa joto lake!
Naapa kwa jua na mwangaza wake! [1]

وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا

Na kwa mwezi unapo lifuatia! [2]

[2] Na kwa mwezi unapo lifuata na likawa nyuma yake kwa kutoa mwangaza baada ya kuchwa jua,
Na kwa mwezi unapo lifuatia! [2]

وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا

Na kwa mchana unapo lidhihirisha! [3]

[3] Na kwa mchana unapo lidhihirisha jua, likaonekana wazi halikufichikana.
Na kwa mchana unapo lidhihirisha! [3]

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا

Na kwa usiku unapo lifunika! [4]

[4] Na kwa usiku unapo lifunika jua, ukawa mwangaza wake hauonekani.
Na kwa usiku unapo lifunika! [4]

وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا

Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! [5]

[5] Na kwa mbingu na kwa Mweza Mtukufu aliye inyanyua na akaijenga kwa hikima yake.
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! [5]

وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا

Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! [6]

[6] Na kwa ardhi na kwa Mweza Mtukufu aliye ikunjua kwa kila upande, na akaitengeneza kwa ajili ya utulivu, na akaifanya kama tandiko.
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! [6]

وَنَفۡسٖ وَمَا سَوَّىٰهَا

Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! [7]

[7] Na kwa nafsi, na aliye iumba na akaiweka sawa, kwa kuipa nguvu,
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! [7]

فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا

Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake! [8]

[8] Akaifunza jema na baya, na akaipa uweza wa kutenda itakayo katika hayo,
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake! [8]

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا

Hakika amefanikiwa aliye itakasa! [9]

[9] Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake kwa ut'iifu na vitendo vya kheri.
Hakika amefanikiwa aliye itakasa! [9]

وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا

Na hakika amekhasiri aliye iviza. [10]

[10] Na hakika amekhasiri mwenye kuzificha fadhila zake, na akayaua matayarisho aliyo umbwa nayo ya kutenda kheri.
Na hakika amekhasiri aliye iviza. [10]

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ

Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, [11]

[11] Kina Thamudi walimkanusha Nabii wao kwa upotovu wao na jeuri zao,
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, [11]

إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا

Alipo simama mwovu wao mkubwa, [12]

[12] Alipo gutuka mwovu wao mkubwa kabisa kutaka kumchinja ngamia.
Alipo simama mwovu wao mkubwa, [12]

فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا

Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. [13]

[13] Saleh, Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia: Mwachilieni huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ale maridhawa katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na tahadharini msimzuie maji katika siku yake aliyo wekewa.
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. [13]

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا

Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. [14]

[14] Wakamkadhibisha Mtume wao katika hilo onyo lake, wakamchinja. Mola wao Mlezi akazibomoa nyumba zao kwa sababu ya dhambi zao; akazisawazisha na ardhi!
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. [14]

وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا

Wala Yeye haogopi matokeo yake. [15]

[15] Wala Yeye Mwenyezi Mungu hakhofu matokeo ya adhabu hiyo, kwani hiyo ni malipo ya haki kwa yale waliyo yatenda.
Wala Yeye haogopi matokeo yake. [15]
Footer Include