Header Include

Swahili translation - Rowad Translation Center

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

QR Code https://quran.islamcontent.com/ak/swahili_rwwad

لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ

Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ

Na ninaapa kwa nafsi inayojilaumu!

Na ninaapa kwa nafsi inayojilaumu!

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ

Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?

Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?

بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ

Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!

Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!

بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ

Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilizoko mbele yake.

Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilizoko mbele yake.

يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ

Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ

Basi jicho litakapodawaa,

Basi jicho litakapodawaa,

وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ

Na mwezi utakapopatwa,

Na mwezi utakapopatwa,

وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ

Na likakusanywa jua na mwezi,

Na likakusanywa jua na mwezi,

يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ

Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?

Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?

كَلَّا لَا وَزَرَ

La! Hapana pa kukimbilia!

La! Hapana pa kukimbilia!

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ

Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.

Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.

يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ

Siku hiyo ataambiwa aliyoyatanguliza na aliyoyaakhirisha.

Siku hiyo ataambiwa aliyoyatanguliza na aliyoyaakhirisha.

بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ

Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.

Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.

وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ

Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.

Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.

لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ

Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.

Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.

إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ

Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.

Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.

فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ

Tunapousoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.

Tunapousoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ

Kisha ni juu yetu kuubainisha.

Kisha ni juu yetu kuubainisha.

كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ

Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani.

Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani.

وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ

Na mnaacha maisha ya Akhera.

Na mnaacha maisha ya Akhera.

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ

Zipo nyuso siku hiyo zitakazong'ara.

Zipo nyuso siku hiyo zitakazong'ara.

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ

Zinamwangallia Mola wao Mlezi.

Zinamwangallia Mola wao Mlezi.

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ

Na zipo nyuso siku hiyo zitakazokunjana.

Na zipo nyuso siku hiyo zitakazokunjana.

تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ

Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.

Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.

كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ

La, hasha! (Roho) itakapofikia kwenye mafupa ya koo.

La, hasha! (Roho) itakapofikia kwenye mafupa ya koo.

وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ

Na pakasemwa: Nani wa kumtibu (apone)?

Na pakasemwa: Nani wa kumtibu (apone)?

وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ

Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki.

Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki.

وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ

Na utakapoambatishwa muundi kwa muundi.

Na utakapoambatishwa muundi kwa muundi.

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ

Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!

Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ

Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.

Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.

وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ

Bali alikanusha, na akageuka.

Bali alikanusha, na akageuka.

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ

Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.

Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.

أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ

Ole wako, ole wako!

Ole wako, ole wako!

ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ

Kisha ole wako, ole wako!

Kisha ole wako, ole wako!

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى

Ati anadhani binadamu kuwa ataachwa bure?

Ati anadhani binadamu kuwa ataachwa bure?

أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ

Kwani hakuwa yeye tone la manii lililoshushwa?

Kwani hakuwa yeye tone la manii lililoshushwa?

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ

Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.

Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.

فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ

Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.

Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.

أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ

Je, huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?

Je, huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?
Footer Include