Header Include

Swahili translation - Rowad Translation Center

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

QR Code https://quran.islamcontent.com/ro/swahili_rwwad

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ

Ole wao hao wapunjao!

Ole wao hao wapunjao!

ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ

Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.

Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe.

وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ

Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.

أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa.

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa.

لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ

Katika Siku iliyo kuu.

Katika Siku iliyo kuu.

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Siku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?

Siku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ

Unajua nini Sijjin?

Unajua nini Sijjin?

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ

Kitabu kilichoandikwa.

Kitabu kilichoandikwa.

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo kwa wanaokadhibisha!

Ole wao siku hiyo kwa wanaokadhibisha!

ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ

Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.

Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.

Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Anaposomewa Aya zetu husema: "Ni visa vya watu wa kale!"

Anaposomewa Aya zetu husema: "Ni visa vya watu wa kale!"

كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao waliokuwa wakiyachuma.

Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao waliokuwa wakiyachuma.

كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa mbali na neema za Mola wao Mlezi.

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa mbali na neema za Mola wao Mlezi.

ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ

Kisha wataingia Motoni!

Kisha wataingia Motoni!

ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ

Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyokuwa mkiyakadhibisha.

Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyokuwa mkiyakadhibisha.

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ

Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika Illiyyin.

Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika Illiyyin.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ

Na nini kitakachokujuvya nini Iliyyin?

Na nini kitakachokujuvya nini Iliyyin?

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ

Kitabu kilichoandikwa.

Kitabu kilichoandikwa.

يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ

Wanakishuhudia waliokaribishwa.

Wanakishuhudia waliokaribishwa.

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ

Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.

Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.

تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ

Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,

Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,

يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ

Watanyweshwa kinywaji safi kilichozibwa vyema.

Watanyweshwa kinywaji safi kilichozibwa vyema.

خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ

Kizibo chake ni miski. Na katika hayo na washindanie wenye kushindana.

Kizibo chake ni miski. Na katika hayo na washindanie wenye kushindana.

وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ

Na mchanganyiko wake ni Tasniim.

Na mchanganyiko wake ni Tasniim.

عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ

Chemchemi watakayoinywa waliokurubishwa.

Chemchemi watakayoinywa waliokurubishwa.

إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ

Kwa hakika wale waliokuwa wahalifu walikuwa wakiwacheka walioamini.

Kwa hakika wale waliokuwa wahalifu walikuwa wakiwacheka walioamini.

وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ

Na wanapopita karibu yao wakikonyezana.

Na wanapopita karibu yao wakikonyezana.

وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ

Na wanaporudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.

Na wanaporudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.

وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ

Na wanapowaona husema: Hakika hawa ndio hasa waliopotea.

Na wanapowaona husema: Hakika hawa ndio hasa waliopotea.

وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ

Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.

Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.

فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ

Basi leo walioamini ndio watawacheka makafiri.

Basi leo walioamini ndio watawacheka makafiri.

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ

Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.

Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.

هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Je, makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda?

Je, makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda?
Footer Include