斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。
《古兰经》含义翻译
由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ
Mbingu itakapochanika.
وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ
Na nyota zitakapotawanyika.
وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ
Na bahari zitakapopasuliwa.
وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ
Na makaburi yatakapofukuliwa.
عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ
Hapo kila nafsi itajua ilichotanguliza, na ilichobakisha nyuma.
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ
Ewe mwanadamu! Nini kilichokudanganya ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ
Aliyekuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha.
فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ
Katika sura yoyote aliyoipenda akakujenga.
كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu.
كِرَامٗا كَٰتِبِينَ
Waandishi wenye heshima.
يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ
Wanayajua mnayoyatenda.
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni.
يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Wataingia humo Siku ya Malipo.
وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ
Na hawatoacha kuwamo humo.
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Na nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Tena nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ
Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi nyingine; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.
share_via