Swahili translation - Rowad Translation Center
translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.
وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا
Ninaapa kwa wanaokomoa kwa nguvu.
وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا
Na kwa wanaotoa kwa upole.
وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا
Na wanaoogelea sawasawa.
فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا
Wakishindana mbio kweli kweli.
فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا
Wakidabiri mambo.
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ
Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka.
تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ
Kifuate cha kufuatia.
قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ
Siku hiyo nyoyo zitapigapiga.
أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ
Macho yatainama chini.
يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ
Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ
Hata tukiwa mifupa iliyobunguliwa?
قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ
Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye hasara!
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ
Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu.
فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ
Mara watakuwa kwenye Uwanda wa mkutano!
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى
Mola wake Mlezi alipomwita katika bonde takatifu la Tuwaa, akamwambia:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri.
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Nami nitakuongoza ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Lakini alikadhibisha na akaasi.
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Akakusanya watu akanadi.
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa Mwenyezi Mungu.
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliyeijenga!
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Akainua paa lake, na akaitengeneza vizuri.
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake.
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake.
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Na milima akaisimamisha imara.
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi itakapofika hiyo Balaa kubwa,
يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ
Siku ambayo mtu atakumbuka aliyoyafanya,
وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
Basi ama yule aliyezidi ujeuri,
وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Na akakhiari maisha ya dunia,
فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Kwa hakika Jahannamu ndiyo makazi yake!
وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ
Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Basi huyo, Bustani ya mbinguni itakuwa ndiyo makazi yake!
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا
Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ
Una nini wewe hata uitaje?
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا
Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu.
كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا
Ni kama kwamba wao siku watakapoiona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.
مشاركة عبر