Header Include

Swahili translation - Rowad Translation Center

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

QR Code https://quran.islamcontent.com/ceb/swahili_rwwad

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ

Itakapochanika mbingu.

Itakapochanika mbingu.

وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.

وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ

Na ardhi itakapotanuliwa.

Na ardhi itakapotanuliwa.

وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ

Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake, ikawa tupu.

Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake, ikawa tupu.

وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.

Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza.

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحٗا فَمُلَٰقِيهِ

Ewe mtu! Hakika wewe unafanya matendo kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.

Ewe mtu! Hakika wewe unafanya matendo kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.

فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ

Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia.

Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia.

فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابٗا يَسِيرٗا

Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi.

Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi.

وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورٗا

Na arudi kwa ahali zake na furaha.

Na arudi kwa ahali zake na furaha.

وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ

Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake.

Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake.

فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورٗا

Basi huyo ataomba kuteketea.

Basi huyo ataomba kuteketea.

وَيَصۡلَىٰ سَعِيرًا

Na ataingia Motoni.

Na ataingia Motoni.

إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا

Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.

Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.

إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ

Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.

Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.

بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرٗا

Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona vyema!

Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona vyema!

فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ

Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapokuchwa.

Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapokuchwa.

وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ

Na kwa usiku na unavyovikusanya.

Na kwa usiku na unavyovikusanya.

وَٱلۡقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ

Na kwa mwezi unapopevuka.

Na kwa mwezi unapopevuka.

لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٖ

Lazima mtapanda tabaka kwa tabaka!

Lazima mtapanda tabaka kwa tabaka!

فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Basi wana nini hawaamini?

Basi wana nini hawaamini?

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ۩

Na wanaposomewa Qur-ani hawasujudu?

Na wanaposomewa Qur-ani hawasujudu?

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ

Bali waliokufuru wanakanusha tu.

Bali waliokufuru wanakanusha tu.

وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ

Na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhamiria.

Na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhamiria.

فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Basi wabashirie adhabu chungu!

Basi wabashirie adhabu chungu!

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ

Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usiomalizika.

Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usiomalizika.
Footer Include