ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ
បកប្រែដោយក្រុមមជ្ឈមណ្ឌលរ៉ូវ៉ាតនៃការបកប្រែ ដោយសហការជាមួយសមាគមអំពាវនាវនៅរ៉ាប់វ៉ា និងសមាគមបម្រើមាតិកាអ៊ីស្លាមជាភាសាផ្សេងៗ។
وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا
Ninaapa kwa zinazotumwa kwa upole!
فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا
Na zinazovuma kwa kasi!
وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا
Na zikaeneza maeneo yote!
فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا
Na zinazofarikisha zikatawanya!
فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا
Na zinazopeleka mawaidha!
عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا
Kuwa udhuru au kuonya.
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ
Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ
Wakati nyota zitakapofutwa.
وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ
Na mbingu zitakapopasuliwa.
وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ
Na milima itakapopeperushwa.
وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ
Na Mitume watakapowekewa wakati wao.
لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ
Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ
Kwa Siku ya kupambanua!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ
Na nini kitakachokujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao, siku hiyo hao wanaokanusha!
أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ
Kwani hatukuwaangamiza waliotangulia?
ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ
Kisha tukawafuatilizia waliofuatia?
كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ
Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ
Mpaka muda maalumu?
فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya.
أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا
Walio hai na maiti?
وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Nendeni kwenye adhabu mliyokuwa mkiikanusha!
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu.
وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia.
فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ
Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ
Hakika wacha Mungu watakuwa katika vivuli na chemchemi.
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ
Na matunda wanayoyapenda.
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika ndio kama hivyo tunavyowalipa watendao mema.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ
Na wakiambiwa: "Inameni!" Hawainami.
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
مشاركة عبر