Header Include

Swahili translation - Rowad Translation Center

translated by Rowwad Translation Center, in cooperation with the Islamic Propagation Office in Rabwah and the Association for Serving Islamic Content in Languages.

QR Code https://quran.islamcontent.com/rn/swahili_rwwad

وَٱلۡفَجۡرِ

Ninaapa kwa alfajiri.

Ninaapa kwa alfajiri.

وَلَيَالٍ عَشۡرٖ

Na kwa masiku kumi.

Na kwa masiku kumi.

وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ

Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja.

Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja.

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ

Na kwa usiku unapopita.

Na kwa usiku unapopita.

هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٞ لِّذِي حِجۡرٍ

Je, hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?

Je, hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya kina A'di?

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya kina A'di?

إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ

Wa Iram, wenye majumba marefu?

Wa Iram, wenye majumba marefu?

ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ

Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?

Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?

وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ

Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?

Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?

وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ

Na Firauni mwenye vigingi?

Na Firauni mwenye vigingi?

ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ

Ambao walifanya jeuri katika nchi?

Ambao walifanya jeuri katika nchi?

فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ

Wakakithirisha humo ufisadi?

Wakakithirisha humo ufisadi?

فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ

Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.

Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.

إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ

Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.

Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.

فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ

Ama mtu anapojaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!

Ama mtu anapojaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!

وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ

Na ama anapomjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!

Na ama anapomjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!

كَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ

Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima.

Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima.

وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hamhimizani kulisha masikini.

Wala hamhimizani kulisha masikini.

وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلٗا لَّمّٗا

Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa.

Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa.

وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا

Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.

Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.

كَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكّٗا دَكّٗا

Sivyo hivyo! Itakapovunjwa ardhi vipande vipande.

Sivyo hivyo! Itakapovunjwa ardhi vipande vipande.

وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفّٗا صَفّٗا

Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu.

Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu.

وَجِاْيٓءَ يَوۡمَئِذِۭ بِجَهَنَّمَۚ يَوۡمَئِذٖ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ

Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?

Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?

يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي قَدَّمۡتُ لِحَيَاتِي

Atasema: Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu!

Atasema: Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu!

فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٞ

Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.

Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.

وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٞ

Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.

Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.

يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ

Ewe nafsi iliyotua!

Ewe nafsi iliyotua!

ٱرۡجِعِيٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةٗ مَّرۡضِيَّةٗ

Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umeridhiwa.

Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umeridhiwa.

فَٱدۡخُلِي فِي عِبَٰدِي

Basi ingia miongoni mwa waja wangu.

Basi ingia miongoni mwa waja wangu.

وَٱدۡخُلِي جَنَّتِي

Na ingia katika Bustani yangu.

Na ingia katika Bustani yangu.
Footer Include