Salin sa Wikang Swahili ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin
Pagsasalin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an
Isinalin ito ng isang pangkat ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin sa pakikipagtulungan ng Samahan ng Da‘wah sa Rabwah at Samahan ng Paglilingkod sa Nilalamang Islāmiko sa mga Wika.
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ
Ninaapa kwa mbingu na kinachokuja usiku!
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ
Na nini kitakachokujulisha ni nini hicho kinachokuja usiku?
ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ
Ni Nyota yenye mwanga mkali.
إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ
Hapana nafsi ila inaye mwangalizi.
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ
Hebu na ajitazame mwanadamu ameumbwa kwa kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa.
يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ
Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ
Siku zitakapodhihirishwa siri.
فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ
Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ
Ninaapa kwa mbingu yenye marejeo!
وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ
Na kwa ardhi inayopasuka!
إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ
Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ
Wala si mzaha.
إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا
Hakika wao wanapanga mpango.
وَأَكِيدُ كَيۡدٗا
Na Mimi napanga mpango.
فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا
Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
share_via