斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼
古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
Unamjua anaye kanusha malipo na hisabu ya Akhera?
Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ
Huyo ndiye anaye msukuma yatima,
Ukitaka kumjua basi ni huyo ambaye anaye msukuma yatima kwa nguvu, na anamtumilia mabavu, na anamdhulumu,
Huyo ndiye anaye msukuma yatima,
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala hahimizi kumlisha masikini.
Na wala hahimizi kulishwa masikini.
Wala hahimizi kumlisha masikini.
فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ
Basi, ole wao wanao swali,
Maangamio yatawashukia wanao sali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.
Basi, ole wao wanao swali,
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ
Ambao wanapuuza Sala zao;
Maangamio yatawashukia wanao swali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.
Ambao wanapuuza Sala zao;
ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ
Ambao wanajionyesha,
Ambao huonyesha kwa watu vitendo vyao, ili wapate cheo katika nyoyo za hao watu, na wasifiwe.
Ambao wanajionyesha,
وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ
Nao huku wanazuia msaada.
Na huku wanazuia hisani zao na msaada wao kwa watu
Nao huku wanazuia msaada.
مشاركة عبر