斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼
古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译
إِنَّآ أَعۡطَيۡنَٰكَ ٱلۡكَوۡثَرَ
Hakika tumekupa kheri nyingi.
Sisi hakika tumekupa kheri nyingi za daima katika dunia na Akhera.
Hakika tumekupa kheri nyingi.
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنۡحَرۡ
Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.
Ilivyo kuwa umepewa hayo, basi dumisha Swala kwa Mola wako Mlezi kwa usafi kabisa, na uchinje dhabihu wako kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa aliyo kupa ya ukarimu, na akakukhusisha wewe khasa kwa kukupa kheri.
Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.
إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ ٱلۡأَبۡتَرُ
Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu.
Hakika huyo anaye kuchukia ndiye aliye katika na kila kheri.
Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu.
مشاركة عبر